Friday, 30 March 2012

ZAMARADI AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME


Mtangazaji wa Kipindi cha TAKE ONE cha Clouds TV, Zamaradi Mketema juzikati alijifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Aga Khan na kumshukuru Mungu kwa kuutua mzigo huo salama.
 Zamaradi alisema kipindi chote cha ujauzito wake kuna waliodhani angejifungua kwa operesheni lakini Mungu amekuwa upande wake.
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kuniwezesha kujifungua salama kwa njia ya kawaida. Nafurahi kumpata mtoto huyu wa kiume na huu ni mwanzo wa maisha mapya,” alisema Zamaradi.

No comments: