Tuesday 29 January 2013

ELIZABETH "LULU" MICHAEL AACHIWA KWA DHAMANA LEO



Habari zilizonifika hivi sasa ni kuwa msanii wa movie Lulu Michael tayari amerudi uraiani  baada ya kuachiwa kwa dhamana leo hii katika mahakama kuu jijini Dar. Licha ya kukamilisha kwa masharti yote aliyopewa jana ikiwa ni pamoja na  kutoa milioni 20 kwa wadhamini wawili,  kuripoti kila mwanzo wa mwezi na kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani hapo, Lulu hakufanikiwa kutoka jana hiyo hiyo kwa kile kilichoripotiwa kutokuwepo kwa msajili wakati huo, hivyo kumlazimu kurudi gerezani
Mara baada yakutoka Lulu (katikati)  akiwa mwenye majonzi na furaha akitokwa na machozi wakati msemaji wa familia Msanii Dr Cheni akizungumza . Lulu amewaomba watanzania wote wamuombee maana hii ni dhamana tu na kesi yake bado inaendela.

Wakili wake Ndugu Flugence Massawe amesema kwamba hii ni hatua ya kwanza kwasababu case bado inaendelea. Kwa sasa wanasubiri mahakama itoe tarehe ya Lulu kurudi mahakamani.

No comments:

Post a Comment