Tuesday 2 October 2012

USIKU WA CHID BENZ NDANI YA MAISHA


              Baghdad japokuwa ni mnene lakini aliweza kuimiliki vizuri stage ya maisha club. 
  Izzo busness akionyesha vitu vyake kwa mashabiki wake ndani ya maisha club Jijini Dar ws Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Naweza kusema kwamba msaniii huyu alichokifanya katika stage ya maisha club mpaka mashabiki wakamkubali kilivyo ni pale ambapo aliamua kuimba bila kutumia beat yoyote basi mara watu wote wakasemaa oyoooooooo.
 Tunda man alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao wamekisanua mbaya ile stage ya Maisha Club kama unavyomuona hapo alikuwa akiimba pini lake la Demu sio. 
 Nuru naye alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao walitoa burudani ya kutosha kabisa katika  usiku wa Chid Benz show ndani ya Maisha club Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Bila kusahau ma Cow boy Ngwea naye alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao wamekisanua mbaya ile stage ya maisha club na kukubalika kwa mashabiki.
Quick Racka akionyesha vitu vyake kama unavyomuona mzee wa katika naye alikuwa ni moja kati ya wasaii ambao wamekisanua mbaya ile stage ya maisha club usiku wa kuamkia leo Jijini Dar es Salaam.
                                                                     Country boy
       Sasa ile show ambayo kila mtu alikuwa anaisubiria kwa hamu ndiyo imefika pale alipopanda mtu mzima Chid benz na kuanza kuimba katika stage ya maisha club jijini Dar es Salaam.

No comments: