Monday 9 April 2012

ELIZABETH MICHAEL AKA LULU


Ndugu zangu, 

Ni kazi ngumu kuwa wakili kwa anayeonekana na jamii kuwa ni ' shetani'. Lakini, kwenye hili la kifo cha kusikitisha cha msanii Steven Kanumba kuna haja ya kukaa chini na kutafakari kwa bidii. 

Kuna maswali pia ya kujiuliza juu ya msichana huyu wa miaka 18 ambaye sehemu kubwa ya jamii imeshamuhukumu kuwa ni muuaji.

Kuna hata ambao hawalijui jina lake la kamili, bali, anajulikana kama ' Lulu'.  Jina lake ni
Elizabeth Michael

Simulizi ya Lulu inaonyesha kuwa yeye na Kanumba walikuwa na mahusiano. Na wivu pia umeingia kwenye mahusiano yao. Hivyo basi, ugomvi na hatimaye kifo cha Kanumba.

Uchunguzi kamili haujakamilika. Na kama haujakamilika, basi, Lulu anabaki kuwa ni mtuhumiwa na si muhusika na kifo hicho. Kumwita Lulu muuaji  ni kuharakisha kutoa hukumu isiyo ya haki. Pamoja na machungu yetu, lakini wanadamu tunapaswa kuwa na subira.

Na ukweli unabaki, kuwa Lulu ni mwanadamu kama wewe na mimi. Na kwa yote yaliyotokea, anabaki kuwa ameondokewa na mpenzi wake. Je, ni nani anayemfariji msichana huyu wa miaka 18 aliyeondokewa na mpenzi wake?

Maggid Mjengwa, 
Dar es Salaam. 
0788 111 76

1 comment:

Anonymous said...

Katika waandishi wote wewe ni mmoja wa wachache wenye ujasiri wa kuongea ukweli. Watu wanamuhukumu huyo msichana bila kujua kilichotokea. Kwenye nchi za wenzetu zinazofuata haki za kibinadamu Lulu hakutakiwa hata kutiwa ndani. Ndiyo waligombana, ikapelekea Kanumba kuanguka, kaka yake akamkuta, baadaye akafa. Lulu sio chanzo cha kifo Kanumba. Hatakiwi kuhukumiwa hata kwa kuua bila kukusudia. Kuna muda hata kama mchache ulipita toka waligombana hadI Kanumba alipokufa. Na katika muda huo Lulu hakuwepo. If anything kaka yake anajua nini kilichotokea. Kuhitimisha kila kitu, ripoti ya hospitali ilipotoka Lulu alitakiwa asiwe mtuhumiwa kabisa. Ila mapolisi wetu na maharaja zetu hawajali haki. Angekuwa Lulu ndiyo amekufa kwenye ugomvi huo Kanumba hasingekuwa jela. Tena Lulu angeitwa malaya na watu kusema anastahili. TAMWA na TAWLA sijui kwa nini hawamsaidii. Namuheshimu Keni na Monalisa kwa ubinadamu wanaouonyesha kwa Lulu. Mungu amsaidie haki itendeke.