Friday 3 February 2012

DIAMOND KUFYATUA VIDEO MBILI HIVI KARIBUNI

MSANII wa muziki wa kizazi kipya ndani ya ardhi ya bongo Diamond, amesema  anatarajia kuzitoa video ya nyimbo zake mbili ambazo ni‘Mawazo’ na ‘Nimpende Nani’,ambapo kwa sasa  yupo katika mchakato huo.

Msanii huyu, alisema kuwa nyimbo hizo ndizo zinazomfanya awe bize kwa sasa kwani anahitaji kuzitoa katika kiwango cha kimataifa.

Alisema kuwa zipo nyimbo nyingi ambazo anahitaji kuzifanyia video lakini kutokana na ubora wa kazi hizo, hana budi kufanya hivyo kwani anaamini tangu alipozitoa zimefanya vizuri sokoni kiasi cha kuteka mashabiki wengi.

Hata hivyo msanii huyo aliuzungumzia wimbo wake wa ‘Nimpende Nani’, kwamba aliutunga kwa ajili ya mashabiki wake na siyo kwa maalumu kwaWema Sepetu na Jokate Mwegelo kama ilivyotafsiliwa na watu.

No comments: